Dodoma FM

Vijana watakiwa kupunguza tabia hatarishi

29 November 2021, 1:05 pm

Na; Shani Nicolous.

Vijana wametakiwa kupunguza tabia hatarishi za maisha zinazosababisha kuogopa kupima Virus vya Ukimwi.

Akizungumza na Taswira ya habari mtaalamu wa afya kutoka katika taasisi ya COHASO Teobad Abdon amesema kuwa vijana wengi wanajihusisha na mahusiano na watu zaidi ya mmoja ambapo hali hiyo husababisha hofu kwa vijana husika kuchukua maamzi ya kupima afya.

Naye Calvin Andrew kutoka COHASO pia amesema kuwa unyanyapaa ni njia moja wapo inasababisha watu wengi kuogopa kupima hivyo jamii itambue namna bora ya kuishi na waathirika wa Virus vya Ukimwi ili kuongeza hamasa kwa vijana na watu wa rika zote katika upimaji.

Kaihule Anod kutoka UDOM Health Club amesema kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kuhimiza na kuelimisha watu juu ya umuhimu wa kupima Ugonjwa huo ili kusaidi kizazi kilichopo hatarini katika maambukizi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutafuta njia mpya za ushawishi kwa vijana katika kuhakikisha wanajitokeza kupima na kuongeza nguvu katika mapambano ya kudhibiti maambukizi zaidi.

Itakumbukwa hivi karibuni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa alizundua kongamano la kisayansi la kitaifa kuhusu VVU na UKIMWI jijini Mbeya, na kilele chake ni siku ya ukimwi duniani tarehe mosi disemba mwaka huu, ambapo siku hiyo imebebwa na kauli mbiu isemayo zingatia usawa tokomeza ukimwi tokomeza magonjwa ya mripuko