Dodoma FM

Wanawake wapewe elimu ya kugombea nafasi mbalimbali

26 November 2021, 12:36 pm

Na; Mariam Matundu.

Tume ya taifa ya uchaguzi imeshauriwa kuwa inatoa elimu endelevu ya chaguzi mbalimbali hapa nchi ili kuwezesha wanawake kuelimika zaidi na kujitokeza kugombea nafasi za uongozi zinazojitokeza.

Hayo yamesemwa na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Sofia Mwakagenda ambapo amesema wanawake wengi wanakosa nafasi kwa sababu ya makosa madogo madogo ambayo kama wakipewa elimu vizuri yanaweza kuzuilika.

Nae mbunge wa jimbo la Mhambwe Dr Florence Samizi amesema ni muhimu kuanza kuchukua hatua tangu ngazi ya familia kuwajengea uwezo na kujiamini kwa watoto wa kike hali itakayochochea chachu katika uongozi.

Kwa upande wake afisa kutoka tume ya taifa ya uchaguzi Fausta Mangige amesema ni kweli baadhi ya wagombea wanaopendekezwa na vyama huwa hawakidhi vigezo kwa kuvunja kanuni ndogo ndogo wakati wa kujaza fomu hivyo ni muhimu elimu ikapelekwa.

Tamwa kwa kushirikiana na FEMNET wamekuwa wakifanya mijadala mbalimbali na wadau tofauti tofauti ikiwa na lengo la kuchochea ajenda ya mwanamke na uongozi .