Dodoma FM

Hatimaye Dodoma yapata kituo cha kwanza cha Tv

26 November 2021, 11:50 am

Na; Mariam Kasawa.

kwa mara ya kwanza Mkoa wa Dodoma utakua na kituo cha Tv ambacho kitarusha matangazo yake moja kawa moja kutokea Dodoma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi leseni ya kituo hicho kipya mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kati Boniface Shoo ameitaka Tasnia ya habari pamoja na wafanyakazi wa Dodoma TV kuendelea kudumisha mshikamano huu.

Akipokea leseni hiyo mkurugenzi wa Dodoma media group (DMG) bi Leila Sanga ameomba ushrikiano udumu baina ya waandishi , watu mbalimbali na wafanyakazi wa Dodoma media group ili kuifikisha Dodoma TV mbali na ili iweze kuleta manufaa kwa jamii.

Nae meneja wa Dodoma media group Zania miraji amesema Dodoma TV ilikuwa ni lengo la bodi ya wakurugenzi wa Dodoma fm miaka 11 iliyopita hivyo mchakato ulianza wa kuanzisha kituo cha Dodoma TV na hatimaye umefanikiwa.