Dodoma FM

Wakazi wa Ihumwa waulalamikia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)

22 November 2021, 11:54 am

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Ihumwa Wilaya ya Dodoma mjini wameulalamikia mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF)juu ya vigezo walivyo zingatia katika usajili wa watu wenye uhitaji wa kusaidiawa na mfuko huo.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ihumwa A wamesema wameshangazwa na majina yaliyo pitishwa na mfuko huo baada ya zoezi la kuwasajili wazee na watu wasio jiweza kufanyika katika mtaa huo.

Bw.Wiliamu Njilimuyi ambaye ni mwenyekiti wa mtaa huo amewashauri wananchi ambao wanahisi kuonewa kwa majina yao kukatwa ni vema kufika ofisini na kujaza fomu za malalamiko.

Aidha mtendaji wa mtaa huo Bi. Siwazuri Karikule amesema kuwa kaya 16 ndizo zilizo pendekezwa na TASAF huku majina ya kaya 55 yakionekana kukosa sifa za kusajiriwa katika mfuko huo.

Bi.Karikule ameeleza baadhi ya sifa zilizo amabatanishwa na barua iliyo rejeshwa na majina yaliyo sajiliwa na ambayo hayakusajiliwa ili kutoa ufafanuzi kwa wananchi kufahamu sifa za walengwa wa mfuko huo.

Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umekuwa na dira ya kusaidia kaya zisizo jiweza kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutokukidhi upataji wa chakula Milo mitatu na kushindwa kukidhi huduma muhimu za kijamii Kama kusomesha watoto na huduma za afya.