Dodoma FM

Rais Samia afungua kongamano la kumbukizi ya historia ya Maalim Seif Sharif Hamad

5 November 2021, 1:46 pm

Na; Fred Cheti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Novemba 5 ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa kumbukumbu ya Maisha ya Hayati Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Rais Samia ameipongeza taasisi maalum ya maalimu Seif Foundation iliyoandaa kongamano hilo la kuenzi maisha ya kiongozi huyo .

CLIP 1…RAIS SAMIA

Aidha Rais Samia amewasihi viongozi wa pande zote mbili kushikana na kushirikiana kwa kuendelezea maridhiano ya umoja wa kitaifa ikiwemo kudumisha utamaduni wa kufanya siasa za majadiliano .

CLIP 2…RAIS SAMIA

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi amesema kuwa pengo la Maalimu Seif halitoweza kuzibika kwa jamii ya wanzanzibar na watanzania kiujumla kutokana na itikadi za kiongozi huyo katika kutetea maslahai ya Taifa na wananchi.

CLIP 3..RAIS MWINYI

Kongamano hilo la kuenzi maisha ya Hayati Maalim Seif Sharifu limeandaliwa na taasis ya Maalimu Seif foundation ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili huku Mgeni Rasmi katika kongamano hilo ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu na kauli mbiu ikiwa “UMOJA WA MARIDHIANO KATIKA UJENZI WA ZANZIBAR NA TANZANIA MPYA “