Dodoma FM

Ukosefu wa elimu wapelekea wafugaji kushindwa kupata faida ya mazao ya mifugo yao

4 November 2021, 12:32 pm

Na ;Thadei Tesha.

Wito umetolewa kwa taasisi mbalimbali zinazohusika na kutoa elimu juu ya kuwapa wafugaji elimu ya njia bora za ufugaji kuwa na utaratibu wakuwatembelea wafugaji hususani vijijini.

Taswira ya habari umefanya mahojiano na baadhi ya wafugaji jijini hapa kufahamu elimu juu ya njia bora za ufugaji pamoja na lishe bora kwa mifugo ilivyowafikia wafugaji hao.

Wamesema ukosefu wa elimu ya mbinu bora za ufugaji zimefanya wao kushindwa kupata faida kutokana na mifugo yao ambapo wametoa wito kwa taasisi zinazotoa elimu juu ya suala hilo kuwa na utaratibu wakuwatembelea Mara kwa Mara.

Bw Fredy Hosena ni Mtafiti mkuu kutoka katika taasisi inayojihusisha na kutoa elimu juu ya lishe bora kwa mifugo amesema miongoni mwa changamoto zinazosababisha wafugaji wengi kushindwa kuwapa mifugo yao lishe bora ni pamoja na wafugaji wengi kutozingatia suala la lishe Katika mifugo yao.

Aidha Ametoa wito kwa wafugaji Nchini kuzingatia suala la kuwapa lishe bora mifugo yao kwani lishe bora kwa mifugo ni muhimu kwa afya ya mifugo Jambo litakalofanya wafugaji kunufaika na mifugo yao.

suala la lishe bora kwa mifugo ni moja ya jambo muhimu ambalo wafugaji wanapaswa kuzingatia ili kupata mazao bora ya mifugo yao.