Dodoma FM

Hali ya utoaji na upokeaji chanjo ya uviko 19 inaridhisha

4 November 2021, 11:44 am

Na; Mariam Matundu

Imeelezwa kuwa hali ya utoaji na upokeaji chanjo ya uviko 19 inaridhisha kwakuwa wananchi wamehamasika na wanajitokeza kwa wingi hasa wananchi wanaoishi vijijini .

Aidha wanawake wametajwa kujitokeza kwa wingi katika kupata chanjo hiyo maeneo yote nchini Tanzania.

Mariam Matundu amefanya mazungumzo na Daktari Baraka Nzobo kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto na ameanza kumuuliza tangu chanzo ianze kutolewa hapa nchini muamko wa wananchi kujitokeza kupata chanjo ukoje?