Dodoma FM

Serikali na jamii yatakiwa kutambua umuhimu wa wanahabari ili wawe salama

2 November 2021, 12:21 pm

Na; Fred Cheti.

Ikiwa leo ni siku maalumu ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanahabari Duniani ripoti ya kamati ya kuwalinda wanahabari ulimwenguni(CPJ) inaeleza kuwa Mataifa 13 yamekumbwa na visa vya mauaji ya kikatili dhidi ya wanahabari.

Ripoti kutoka katika kamati hiyo iliyotolewa mwaka jana inaeleza kuwa mauaji hayo yanatekelezwa na vikundi vya uhalifu, viongozi wa kisiasa, na wafanyabiashara kwa lengo la kuficha uovu wao.

Taswira ya habari imezungumza na Bw.Proseper Kwigize ambae ni mwenyekiti wa mtandao wa redio za kijamii Tanzania ambae pia anafanya kazi na shirika la utangazaji la ujerumani (DW ) anasema kuwa mwanahabari ili awe salama ni lazima serikali na jamii kutambua umuhimu wake na mwandishi mwenyewe ni lazima ahakikishe anazingatia weledi pamoja na maadili katika taaluma yake

Aidha Bw. Prosper ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuacha kuagopa na kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia taratibu zote za kitaaluma pamoja na kujifunza mambo mapya kwa kuandika habari zenye matokea katika jamii

Pia amezitaka mamlaka zinazotunga sera na sheria kuacha kuwaona waandishi wa habari kama maadui pale ambapo wanafichua wanayofanya ambayo ni kinyume cha mila na desturi za kitanzani.

Mwanahabari kama nyenzo muhimu ya Mawasilano anapaswa kulindwa na kuthaminiwa na hivyo serikali jamii,pamoja na wadau mabalimbali ni lazima wahakikishe wanatoa ushirikiano katika kulinda taaluma hiyo.