Dodoma FM

Baraza la Madiwani Jijini Dodoma lampongeza rais Samia Suluhu Hassan

28 October 2021, 12:43 pm

Na; Alfred Bulahya.

Baraza la madwani wa Jiji la Dodoma limempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kwa kulipatia fedha kiasi cha shilingi, billion 2, million 974 ,laki 672 na 970.48, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mpango wa maendeleo ya ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.

Pongezi hizo zimetolewa leo katika kikao cha baraza hilo ambapo madiwani kwa nyakati tofauti wamempongeza Rasi Samia na kuahidi kuzisimamia kama ilivyo elekezwa.

INSERT….MADIWANI CLP 1.

Hata hivyo wamewaomba watendaji na wasimamizi wengine kuamua, kupanga na kusimamia kwa pamoja huku wakiwasihi viongozi wanaohusika na ugawaji fedha hizo kuwahisha mchakato wa ugawaji ili uendane na muda uliopangwa katika utekelezaji wa miradi inayolengwa.

insert…….MADIWANI CLP 2

Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri, katika kikao hicho amewataka madiwani kwenda kusimamia maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kwa kuacha kujiingiza katika kamati za utekelezaji ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

insert…..DC DOM MJINI CLP 2

Katika mgawanyo wa fedha hizo, billion 2 milioni 860 zimeelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa143 ya sekondari, milioni 80, madarasa 4 ya vituo shikizi milioni 34 laki 672 na 970. 48, zikielekezwa katika kampeni dhidi ya chanjo ya uviko 19.