Dodoma FM

Spika Ndugai azitaka Asasi za kiraia nchini kutatua changamoto za watanzania na sio kutumika

23 October 2021, 2:39 pm

Na;Mindi Joseph .

Spika Wa Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh.Job Ndugai amezitaka Asasi Za Kiraia Nchini kutokutumika na badala yake zifanye Kazi Kwa Weledi na Uadilifu.

Akizungumza Leo Jijini Dodoma Spika wa Bunge Job Ndugai wakati wa Ufunguzi Wa Wiki Ya Azaki (2021)   Amesema Asasi za kiraia Hazina Budi Kutafuta Fedha Ndani Na Nje Ya Nchi  Kwa Ajili Ya Kuleta Tija  Na Vipaumbele Vya Taifa, pamoja na Kutumia Tafiti  Na Takwimu Zitazosaidia Kutoa Majawabu Ya Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Watanzania .

Mh Ndugai ameongeza kuwa Asasi zinatakiwa kuwa na Mwenendo Wa Kukosoa Viongozi Wa Serikali pamoja na Kuwapongeza Wanapofanya Vizuri utekelezaji wa Majukumu Yao Kwa Ajili Ya Maslahi Ya Watanzania Wote.

Kwa Upande Wake Rais Wa Fcs Dkt Stigmata Tenga amesema Bunge linawajibu wa kuleta Mabadiliko Chanya Na  Kupitia Upya Sheria ,Taratibu Na Miongozo Ambayo Inaziongoza Asasi Hizo  Ili Ziweze Kushiriki Vyema Katika Maendeleo Ya Taifa.

Naye  Mkurugenzi  Mtendaji Wa (Wajibu ) Ludovick Utoh  amesema AZAKI ni Zaidi ya mashirika.

Maonyesho Ya Wiki Ya Azaki Kwa Mwaka (2021) yameanza leo na octoba 23 na Yanakwenda Sambamba Na Kauli Mbiu Isemayo Azaki Na Maendeleo.