Dodoma FM

Jamii yaaswa kuacha tabia ya kutelekeza watoto ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani

22 October 2021, 11:54 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa jamii kuacha tabia ya kutelekea watoto ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.

Wito huo umetolewa na mwanaharakati kutoka shirika lisilo la kiserikali la Kisedeti Ibrahm Mtangoo amesema kuwa wimbi kubwa la watoto wa mitaani limetokana na wazazi kutelekeza watoto kwa sababu mbalimbali za kimaisha.

Amesema kuwa vijana wanatakiwa kufahamu aina ya maisha ya kimahusiano yanayoanzishwa ili kuepusha mimba zisizotarajiwa hata hivyo amehimiza vijana kuzingatia elimu ya afya a uzazi ambayo itakuwa msaada mkubwa kupunguza utlekezaji wa watoto.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa sababu ya utelekezaji wa watoto hutokea pale mzazi mmoja anapokataa kushiriki katika malezi hivyo wameomba mashirika mbalimbali na serikali kuendelea kutoa elimu kwa vijana .

Ili kupunguza wimbi la watoto wa mtaani serikali inatakiwa kuchukua hatua kali kwa mzazi yoyote atakayebainika na tuhuma za utelekezaji wa Mtoto pamoja na utolewaji wa elimu ya kutosha juu ya afya ya uzazi.