Dodoma FM

Waendesha vyombo vya moto jijini Dodoma watakiwa kufuata taratibu na kanuni za usalama barabarani.

21 October 2021, 12:30 pm

Na; Shani Nicolous.

Waendesha vyombo vya moto jijini Dodoma wametakiwa kufuata taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha usumbufu wa adhabu zitakazolewa kisheria.

Akizungumza na Dodoma fm kupitia kipindi cha Dodoma live rais wa jumuiya ya wananfunzi wanaosoma sheria chuo kikuu cha Dodoma Gidius Kato amesema kuwa kuna makosa ambayo kisheria yana adhabu zake kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wanapofanya makosa barabarani.

Amesema kuwa ajali nyingi za barabarani zinasababishwa na masuala madogomadogo yanayoweza kukemewa na kuachwa kama matumizi ya pombe wakati wa kuendesha chombo cha usafiri .

Hata hivyo amekishukuru kituo hiki kwa kutoa elimu zenye kufungua watu na kuahidi ushirikiano ulioshiba kuhamasisha mabadiliko zaidi katika jamii hasa upande wa sheria.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa ni wajibu wa kila mtumiaji wa barabara na usafiri wake kuzingatia sheria za usalama barabarani kwani sheria haiwezi kuvumilia ajali zinazoweza kuzuiliwa.

Suala la uhai ni haki ya kila Mtanzania hivyo watumiaji wa vyombo vya usafiri wanatakiwa kuongeza umakini ili kulinda haki za watanzania wanaotumia vyombo vya usafiri