Dodoma FM

Ukarabati wa barabara katika kata ya mnadani utapunguza usumbumbufu kwa wakazi wa eneo hilo

21 October 2021, 2:05 pm

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa endapo ukarabati wa barabara unaoendelea katika mtaa wa Karume Kata ya Mnadani jijini Dodoma utakamilika utapunguza usumbufu kwa wakazi hao hususani kipindi Cha Mvua.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo wakati wakizungumza na taswira yahabari mara baada ya kuanza kwa ukarabati wa barabara zilizopo katika mtaa wa Karume.
Waamesema barabara za mtaa huo zimekuwa korofi kwani kipindi cha mvua zinapitisha maji ambayo yamekuwa yakibomoa nyumba.

Matwiga Kiatya ni mwenyekiti wa mtaa wa Karume amesema barabara hizo zilikuwa zimeharibika kupita kiasi lakini hivi sasa ukarabati umeanza.

Amesema lengo walilonalo baada ya kumalizika kwa ukarabati wataongea na LATRA ili daladala zianze kupita eneo hilo kutoka Dodoma mjini kuelekea mnadani kwani mtaa huo unawatu wengi.

Barabara zilizopo katika mtaa wa Karume Kata ya Mnadani Jijini Dodoma zimekuwa zikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwa muda mrefu kwani kipindi cha mvua hazipitiki kirahisi hivyo kusababisha kukwama kwa shughuli za kiuchumi.