Dodoma FM

Wakazi wa kata ya Chigongwe walalamikia uhaba wa nyumba za walimu na uchache wa walimu katika shule ya msingi

20 October 2021, 12:24 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Chigongwe Wilaya ya Dodoma mjini wamelalamikia ukosefu wa nyumba za walimu pamoja idadi ndogo ya walimu katika shule ya msingi Ngh’ambala

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza nataswira ya habari wamesema kuwa changamoto ni idadi kubwa ya wanafunzi ambayo haienani na idadi ya walimu walioopo ambao nao hawana nyumba za kuishi

Mwenyekiti wa mta wa Ngh’ambala Bw.Wiliamu Nado amekili shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu pamoja na nyumba zao hata hivyo uchakavu wa majengo ukiwa ni adha nyingine

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Simoni Machela amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo licha ya kuendelea na hamasa kwa wanachi kujenga baadhi vyumba ili kuwapunguzia umbali mrefu kwa baadhi ya wanafunzi

Mazingira ya kufundishia mashuleni ikiwa ni pamoja na walimu,nyumba za walimu na vyumba vya madarasa imekuwa chachu ya ufaulu kwa wanafunzi