Dodoma FM

Wakazi wa Mkoka walalamika kuendelea kukosa huduma ya maji

19 October 2021, 11:32 am

Na; Selemani Kodima.

Licha ya kuchimbiwa visima vya maji ,Bado wananchi wa kijiji cha mkoka wilayani kongwa wamelalamika kuendelea kupata changamoto ya maji baridi.

Akizungumza kwa Niaba ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoka Bw Elia Chibago amesema baada ya ziara ya Waziri wa Maji kupita hatua iliyofuta walichimbiwa kisima cha maji baridi lakini hadi sasa wameshindwa kusambaziwa bomba za maji.

Amesema kuwa Imani yao ni kubwa Iwapo Wakala wa usambazaji wa maji Vijijini RUWASA akiwatembelea kwa ajili ya kwenda kukamilisha miundombinu ya maji kwa utandazaji wa Bomba za maji pamoja na vichoteo.

Pamoja hayo amesema hatua walizochukua ni kufikisha malalamiko ya wananchi kwa diwani wa kata hiyo ambapo wamepewa ahadi ya ufatiliaji ili kujua lini watamaliziwa changamoto hiyo.

Ni miezi mitatu imepita Tangu wachimbiwe kisima cha Maji lakini wamebakia kuwa watazamaji wa kisima hicho huku wakiwa na matamanio makubwa ya kupata huduma ya maji baridi ili kupunguza adha ya maji katika eneo lao.