Dodoma FM

Vyombo vya habari vimetakiwa kuboresha mwonekano wa watafsiri wa lugha za alama.

19 October 2021, 10:58 am

Na; Thadei Tesha.

Vyombo vya habari vimeshauriwa kutoa kipaumbele kwa Watu wenye ulemavu wa kutosikia kwa kuboresha mwonekeno wa watafsiri wa lugha ya Alama.

Wito huo umetolewa na Bi Joyce Masha ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Foundation for disability ambalo linahuska na kuwatetea Watu wenye ulemavu hususani kwa makundi ya watoto vijana na wazee.

Amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwa mstari wa Mbele Katika kuwatumia wakalimani wa lugha ya Alama ili kutoa nafasi kwa kundi hilo kupata uelewa juu ya masuala mbalimbali kutokana na uchache wa wakalimani Katika vyombo vingi vya habari.

Aidha Ametoa wito kwa jamii kujifunza lugha ya Alama ili kurahisisha mawasuliano baina ya jamii na kundi hilo la Watu wenye ulemavu wa kutosikia.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuna umuhimu wa vyombo vya habari kutoa kipaumbele kwa kuweka wakalimani wa lugha ya Alama Kwani kundi hilo limesahaulika Katika jamii.

Lugha ya Alama imekuwa na umuhimu Katika jamii kutokana na kuwa na mchango mkubwa husuaani kwa kundi la Watu wasiosikia hivyo jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia kundi hilo.