Dodoma FM

Mafundi wa simu za mkononi wametakiwa kuacha tabia ya kuflash simu kwa lengo la kuondoa ulinzi kwani ni kinyume cha sheria

15 October 2021, 11:47 am

Na; Benard Filbert.

Mafundi wanaotengeneza simu za mkononi zilizoharibika wameombwa kuacha tabia ya kuflash simu kwa lengo la kuondoa ulinzi kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya makosa ya mitandao.

Hayo yameelezwa na Bi Rachel Charles katibu wa kamati ya uelimishaji kutoka mamlaka ya mawasiliano kanda ya kati wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu athari za kuflash simu.

Bi Rachel amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya mafundi wa simu za mkononi kuflash simu kitu ambacho kinasababisha kupoteza namba za utambuzi wa simu husika (IMEI NUMBER)

Amesema sheria inakataza kitendo cha watu kuflash simu hali iliyosaidia kupungua kwa vibanda ambavyo vilikuwa vikifanya hivyo.

Baadhi ya watumiaji wa simu za mkononi wamesema ni vyema serikali ikaendelea kusimamia vizuri sheria zinazokataza kufanya vitendo hivyo ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 inaeleza kuwa Kuflash simu ni kosa la jinai; adhabu inaweza kuwa faini isiyopungua milioni 30 au kifungo kisichozidi miaka 10.