Dodoma FM

Elimu ya kujikinga na uviko 19 yawafikia wananchi wa vijijini Mkoani Dodoma

12 October 2021, 1:14 pm

Na;Yussuph Hans.

Jitihada za kufikisha Elimu ya kuchukuwa tahadhari na kujikinga dhidi ya Ugonjwa unaoenezwa na Virusi vya korona UVIKO-19, inaelezwa elimu hiyo imewafakiwa vyema hadi wakazi wa maeneo ya vijiji mbalimbali Mkoani Dodoma.

Hayo yanajiri kufuatia Taswira ya Habari kuzungumza na wakazi wa maeneo ya baadhi ya vijiji Mkoani hapa na kukiri kufahamu juu kujilinda dhidi ya Ugonjwa huo.

Aidha wameongeza kuwa kutokana na athari mbalimbali za Ugonjwa huo kiuchumi na kiafya, Serikali haina budi kuongeza nguvu ya kutoa Elimu kuvifikia Vijiji vingi zaidi.

Taswira ya habari imezungumza na Diwani wa Kata ya Mlowa Barabarani Mh Anjelo Lucas ambapo amesema kuwa wamekuwa na desturi ya kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo maeneo yenye mikusanyiko ya watu, juhudi ambazo kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda.

Serikali imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha inafikisha elimu ya Ugonjwa wa virusi vya Korona (UVIKO-19) Nchini nzima ambapo pia wanashirikiana na Viongozi wa vijiji husika kufikisha elimu kwa lugha za asili ya maeneo hayo.