Dodoma FM

Wananchi washauriwa kuepuka matumizi ya pombe yaliyo pitiliza

11 October 2021, 12:45 pm

Na; Benard Filbert.

Jamii imeshauriwa kuacha kunywa pombe kupita kiasi ili kuepusha athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo matatizo ya akili.

Hayo yameelezwa na Bi. Gladnes Munuo katibu mkuu kutoka taasisi ya TAANET ambayo inahusika na kupinga unywaji wa pombe kupita kiasi wakati akizungumza na taswira ya habari.

Bi. Gladnes amesema unywaji wa pombe kupita kiasi unaathari nyingi katika afya ya binadamu ikiwemo homa ya ini pamoja na magonjwa mbalimbali ya akili.

Aidha amesema kuwa pombe zote za viwandani na za kienyeji zinaathari hivyo jami inatakiwa kutambua madhara yatokanayo na pombe hizo.

Baadhi ya wananchi wamesema ni vyema Serikali ikatoa maelekezo ya kiwango sahihi cha unywaji wa pombe ili kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakitumia pombe kupita kiasi.

Tarehe 10 October ilikuwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga unywaji wa pombe kupita kiasi ambapo maadhimisho hayo yalifanyika katika hospital ya afya ya akili Mirembe Mkoani Dodoma huku jamii akiaswa kupinga unywaji pombe kupita kiasi.