Dodoma FM

Mkoa wa Dodoma unaongoza kwa kutoa chanjo ya uviko 19

4 October 2021, 1:44 pm

Na; Selemani Kodima .

Imeelezwa kuwa mkoa wa Dodoma unaongoza kwa utoaji chanjo ya Ugonjwa wa Uviko -19 ambapo kati ya chanjo Elfu Hamsini ambazo zilitolewa kwa ajili ya Ugonjwa Uviko-19 ,tayari chanjo elfu thelathini zimetumika .

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala mkoa wa Dodoma Dkt Fatma Mganga wakati akitoa wito kwa wazee pamoja na Jamii kuchanja chanjo ya Uviko 19 ambapo amesema tangu kuzinduliwa kwa chanjo hiyo tarehe 3 mwezi wa nane mpaka leo chanjo Elfu 30 kati ya Elfu elfu 50 zimeshatolewa.

Dkt Mganga amesema mkoa wa dodoma umekuwa kinara hapa nchini kutokana na wananchi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko 19 .

Aidha amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kupata chanjo ya Uviko -19 ili kufanikisha kumalizika kwa Chanjo zote Elfu hamsini.

Akizungumzia kundi la Wazee Dkt Mganga amesema kundi la wazee lipo hatarini kupata Ugonjwa wa uviko-19 hivyo ni Wajibu wa wazee kwenda kupata chanjo hiyo ili kupunguza hatari hiyo.

Pamoja na hayo amesema serikali inatarajia kupokea Dozi Milioni 2 za Sinopharm kutoka Nchini China. Kwenye chanjo hiyo, mtu atapokea dozi mbili tofauti na Johnson & Johnson ambayo inachomwa mara moja.