Dodoma FM

Waziri mkuu awataka viongozi wa Dini na waumini kuacha kutumia majukwaa ya dini kuhubiri siasa

1 October 2021, 1:04 pm

Na; Fred Cheti.

Serikali imesema kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi zote za dini nchini zenye nia safi na thabiti katika kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya kijamii na kiroho yenye manufaa kwa umma inafanikiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba mosi na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa wakati akizindua Msikiti wa Jamiu uliopo Ikwiriri wilayani Rufiji ambapo amewataka viongozi wa dini pamoja na waumini wa dini zote nchini kuacha kutumia majukwaa ya dini kwa masuala ya kisiasa badala yake wazidi kulinda amani ya nchi.

Aidha Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watanzania kuacha kuchukulia kwa mzaha suala la ugonjwa wa Uviko 19 badala yake waendelee kusikiliza ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya nchini pamoja na kuchukua tahadhari zote kwa kuwa ugonjwa huo upo nchini.

Kwa upande Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abukakary Bin Zuberi ameishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini huku akiwataka waumini wa dini ya kiisalamu pamoja na wasio wa dini hiyo kuendelea kusikiliza ushauri unaotolewa na viongozi wa nchi pamoja na wataalamu wa afya juu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo amabao umekua tishio kwa sasa duniani