Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za asasi zisizo za kiserikali

1 October 2021, 12:49 pm

Na; Nadhiri Hamisi.

Wito umetolewa kwa wananchi kuunga mkono juhudi za asasi zisizo za kiserikali kwa kufuata huduma zinazotolewa na asasi hizo ili kuleta maendeleo nchini.

Hayo yameelezwa na Bwana Jacob kessy Mkurugenzi wa shirika la youth royal empowerment organization la jijini Mwanza na kuongeza kuwa ili maendeleo yafikiwe nchini ni lazima wananchi wapate uhakika wa huduma zote kutoka katika taasisi za serikali na asasi zisizo za kiserikali.

Bwana kessy aliwataka vijana wanaoanzisha mashirika yasiyo ya serikali kutoa huduma kwanza na sio kuwaza maslahi binafsi jambo linalopelekea asasi nyingi zisizo za kiserikali kuacha kutoa huduma lengwa.

Aidha baadhi ya wananchi jijini Dodoma wamesema kuwa elimu inapaswa kutolewa zaidi ili watu wa kawaida watambue umuhimu wa asasi hizo kwani wengi wao wanauelewa fiinyu na kuwataka waanzilishi wa asasi hizo kutoa huduma zao kwa weledi unaohitajika..