Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujifunza lugha ya alama ili iweze kutatua changamoto baina yao na viziwi

24 September 2021, 10:17 am

Na;Mariam Matundu.

Ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya viziwi ,jamii imetakiwa kutambua kuwa lugha ya alama ni lugha kama zilivyo lugha zingine na jamii ione umuhimu wa kujifunza ili kutatua changamoto ya mawasiliano baina yao na viziwi.

Bwana Frank Sarungi ni kiziwi anayeishi jijini Dodoma akitafsili mkalimani wa lugha ya alama amesema kuwepo kwa siku ya lugha ya alama kunaleta matumaini kwa viziwi na kupata imani kwamba lugha hiyo inakuwa.

Clip 1frank………………..

Amesema ipo haja kwa serikali kuweka msingi wa kufundisha lugha ya alama kama somo la lazima katika vyuo mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha masasiliano pindi wanapohitaji huduma mbalimbali.

Clip 2 frank………………

Kwa upande wake mkalimani Adrian Chiyenje amesema amekuwa amekuwa akikutana na changamoto katika jamii ambapo wengi hushangaa wanapomuona anaongea kwa alama.

Clip 3 mkalimani…………………

Wiki ya viziwi imeanza kuadhimishwa tangu sept 20 na itafika kilele sept 26 ambapo maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika jijini mwanza yakiwa na kaulimbiu isemayo UKUSHEHEREKEA USTAWI WA JAMII YA VIZIWI.