Dodoma FM

Wazazi wametakiwa kuwapa mafunzo ya ziada wahitimu wa darasa la saba ili kuwaepusha na vitendo hatarishi

21 September 2021, 12:08 pm

Na ; Thadei Tesha.

Wazazi jijini hapa wameshauriwa kuhakikisha wanawasaidia watoto wao waliohitimu darasa la saba katika kuwawezesha kupata mafunzo mbalimbali katika kipindi hiki wanachosubiri matokeo ili kupunguza vitendo vya ukatili na watoto kuharibikiwa kimaadili katika jamii.

Akizungumzia athari ambazo zinaweza kuwapata watoto pindi wawapo mtaani bila ya shughuli yoyote mtaalamu wa saikolojia bw muhibu mtahu amesema watoto wengi wamekuwa wakijiingiza katika vitendo hatarishi kutokana na wazazi wengi kutokuwa karibu nao ambapo ametoa wito kwa wazazi kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watoto hao.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na wanafunzi waliohitimu darasa la saba jijini hapa wamesema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakihusika katika kuwaharibu watoto wao kimaadili ambapo wametoa wito kwa wazazi kuacha vitendo hivyo na badala yake kuwapa elimu kama kipaumbele.

Miongoni mwa visababishi vikubwa vya kuharibika kwa maadili kwa watoto vimekuwa vikisababbishwa na wazazi kutowatengenezea watoto wao mazingira bora katika jamii ambapo jamii zinapaswa kushirikiana kukomesha vitendo hivyo.