Dodoma FM

Serikali yaombwa kutoa kipaumbele kikubwa cha bajeti na sera ili kusaidia maendeleo ya elimu maalum

21 September 2021, 12:34 pm

Na;Mindi Joseph.

Serikali imeombwa kutoa kipaumbele kikubwa cha bajeti na sera katika kuanzisha na kuendeleza shule jumuishi kwa watoto ili kusaidia maendeleo ya elimu maalumu.

Akizungumza na taswira ya habari Msimamizi wa Sera kwenye Mradi wa Elimu Jumuishi unaotekelezwa Mkoani Dodoma Fredrick Mkatambo amebainisha kuwa ili kuhakikisha watoto wote wanajumuishwa bila kujali tofauti zao au ugumu wa kujifunza.

Ameongeza kuwa Watoto wenye ulemavu wana haki ya kufurahia haki ya kupata elimu kama watoto wengine na ameiomba jamii kutoa taarifa kwa vyombo vya kisheria pale inapoona watoto wananyimwa haki zao.

Wazazi pia wameendelea kuhimiza watoto wenye uhitaji maalum kutowaficha ndani.

Mnamo mwaka 2004 Tanzania ilitoa Sera ya Kitaifa ya huduma kwa watu wenye ulemavu, 2004 inayotoa wazi upatikanaji wa elimu ya msingi kwa watoto wote na wale wenye ulemavu watapewa kipaumbele na kutunga Sheria ya Watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 ambayo inaainisha juu ya haki ya elimu kwa Watoto wenye ulemavu Pamoja na Mkakati wa Kitaifa wa elimu jumuishi mwaka 2017.