Dodoma FM

Uelewa hafifu juu ya sheria za usafi wa mazingira unachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira

17 September 2021, 1:54 pm

Na ;FRED CHETI .

Inaelezwa kuwa uelewa hafifu kuhusu sheria ndogo za usafi wa mazingira na rasilimali za asili umekua ukichangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira katika jamiii.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakazi Jijini Dodoma wakati wakizungumza na taswira ya habari ambapo wamesema licha ya sheria hizo kuwekwa katika kila kata lakini si kila mwananchi ana uelewa wa sheria hizo hivyo Serikali ni vyema ikaweka utaratibu ambao utasaidia kila mwananchi kufikiwa na elimu hiyo.

Kwa upande wake Bw. Kapesa Youngson ambae Mtaalamu wa mazingira kutoka shirika la RUTI amesema kuwa mwananchi kutokujua sheria hizo hakumfanyi kuondokana na adhabu zinazotolewa kutokana na uchafuzi wa mazingira kwa kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kufatilia sheria hizo zinazotungwa na Halmashauri kwa kuwa zinatungwa kwa mjibu wa sheria.

Sheria Ndogo zinajulikana kama Sheria za Hifadhi za Mazingira ambazo hutungwa na kila Halmashauri Nchini ambazo hutumika katika eneo lolote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri husika.