Dodoma FM

Imeelezwa kuwa usawa wa kijinsia katika uongozi mbalimbali hapa Nchini unawezekana

14 September 2021, 1:58 pm

Na; Mariam Matundu.

Imeelezwa kuwa usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini unawezekana kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassani anaonesha nia ya dhati katika kufikia hilo kutokana na teuzi mbalimbali anazozifanya.

Hayo yameelezwa na mratibu wa mradi wa ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya kisiasa Dorothy otieno wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi na nafasi ya mwanamke katika siasa kwa vijana yanayofanyika jijini Dodoma .

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanawake na kuongeza idadi ya wanawake viongozi katika ngazi mbalimbali hapa nchini.

Nae mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben amesema wamefanikiwa kuongeza uchechemuzi katika masuala ya uongozi kwa wanawake ambapo jumla ya wanawake wanaharakati vijana 55 wameunganishwa na washauri ili kuelekezwa kuhusu masuala ya siasa pamoja na kukutana na watunga sera .

Baadhi ya wanawake viajana waliohudhuria mafunzo hayo wamesema bado wanawake hawajiamini katika kugombea nafasi za uongozi hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuamsha ari kwa wanawake katika kugombea nafasi hizo.

Chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na kituo cha usuluhishi (CRC )pamoja na young and alive Initiative (YAI)kwa pamoja na shirika la mawasiliano barani Afrika (FEMNET) wamewakutanisha wanawake vijana 30 katika mafunzo ya siku nne kuanzia leo sept 14 hadi sept 17 kwa lengo la kuongeza idadi ya wanawake viongozi.