Dodoma FM

Rais Samia awataka mawaziri wapya kwenda kufanya kazi kwa bidii

13 September 2021, 12:57 pm

Na; Fred Cheti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu amewataka mawaziri wapya aliowateua siku ya jana kwenda kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika wizara walizochaguliwa na kwa watanzania kwa ujumla.

Rais Samia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la uapisho wa Mawaziri hao wateule ambapo amesema kuwa ana imani kuwa uteuzi huo utaenda kuleta mabadiliko chanya katika wizara pamoja na kwa watanzania kutokana na uzoefu waliokuwa nao viongozi hao.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa ambae ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria tukio hilo amewapongeza mawaziri hao kwa kuchaguliwa katika nafasi hizo na amesema kuwa wana jukumu kubwa la kutekeleza maagizo wanayopewa ili kutimiza azma ya serikali ya kuwatumikia wananchi.

Katika hatua nyingine Spika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania Mh. Job Ndugai amewakaribisha mawaziri hao bungeni ambapo amesema kuwa bunge litawapa ushirikiano wa kutosha katika mambo yote ya kuisaidia serikali .

Mawaziri walioteuliwa ni pamoja na Mh. January Makamba ambae ameteuliwa kuwa waziri wa nishati,Mh Makame Mbarawa ambae anaenda katika wizara ya ujenzi na uchukuzi,Dkt Stergomena Tax amekuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa pamoja na Dkt. Ashatu Kijaji ambae atahudumu katika wizara ya habari ya mawasiliano na teknolojia.