Dodoma FM

Wazee waliopo katika makazi ya wazee Sukamahela wilayani Manyoni waishukuru serikali kwa kukarabati makazi yao

6 September 2021, 12:12 pm

Na; Mariam Matundu.

Katika kuelekea siku ya wazee duniani wazee wanaoishi katika makazi ya wazee sukamahela wilayani manyoni wameishukuru serikali kwa kufanya ukarabati katika majengo ya makazi hayo ikiwa ni pamoja na wazee hao kupata uhakika wa chakula kila siku .

Akizungumza mbele ya waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto ,afisa mfawidhi wa makazi ya wazee suka mahela Twaha Faraji Kibulula amesema maboresho hayo yamepunguza changamoto kwa wazee katika makazi hayo.

Aidha amesema pamoja na hayo makazi hayo bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa mtaalamu wa maabara pamoja na gari la kituo

Dkt Dorothy Gwajima ni waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya manyoni kupeleka mtaalamu wa maabara katika zahanati ya sukamahela inayohudumia wazee hao .

Waziri Gwajima amesema katika kuendelea kuboresha huduma kwa wazee serikali ipo katika hatua za mwisho za kufanya mapitio ya sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 ambapo masula muhimu yamewekewa mikakati mathubuti.

Kwa mujibu wa ripoti ya taifa ya makadilio ya watu ya mwaka 2013 hadi 2020/2035 kwa mwaka 2021 Tanzania inakadiliwa kuwa na wazee zaidi ya milioni mbili .

October mosi kila mwaka huadhimishwa siku ya wazee Duniani ambapo kwa mwaka huu yakiwa na kaulimbiu isemayo matumizi sahihi ya kidijitali kwa ustawi wa rika zote.