Dodoma FM

Serikali imesema itaendelea kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari na kuchanja chanjo ya Uviko 19

6 September 2021, 11:48 am

Na; Selemani Kodima.

Serikali imesema itaendelea kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari na kuchanja chanjo ya Uviko 19 huku pia wakiendelea kuhamasisha kutumia njia nyingine za kujikinga na Ugongwa huo.

Akizungumzia Umuhimu wa wananchi kuchanja chanjo ya Uviko -19 Dkt Baraka Nzobo kutoka wizara ya afya ,idara ya kinga amesema chanjo ni njia bora ya kujikinga na virusi vya Corona hivyo jamii waendelee kuchukua maamuzi ya kuchanja .

Dkt Nzobo amesema licha ya chanjo kuendelea kutolewa lakini jamii wanapaswa kuendelea kujikinga kupitia njia nyingine ambazo wamekuwa wakishauri ili kujikinga na virusi vya ugongwa wa Uviko -19.

clip 1

Aidha akizungumzia njia ya matumizi ya tiba asilia Dkt Nzobo amesema kupitia sera ya afya ya mwaka 2007 imeanisha umuhimu wa tiba mbadala ,tiba asilia na ukunga wa jadi hivyo ni sehemu ya juhudi ambazo serikali walitumia kwa ajili ya kuwalindaa wananchi wake.
Pamoja na hayo amewashauri wananchi kwa wale wenye umri kuanzia miaka 18 kujitokeza kwenda kupata chanjo ili kujilinda na ugonjwa wa Uviko -19.