Dodoma FM

Kata ya Masanga yaiomba serikali kuwasaidia kuongeza vyumba vya madarasa

1 September 2021, 12:55 pm

Na; Victor Chigwada.

Licha ya jitihada za wananchi wa Kata ya Msanga Wilayani Chamwino katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa wameiomba Serikali kuwaongezea nguvu ya ujenzi wa madarasa pamoja na walimu

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na upungufu wa walimu imekuwa changamoto kubwa licha ya matokeo mazuri katika shule zao

Mwenyekiti wa Kijiji cha Msanga Bw. Khatibu Ramadhani amesema licha ya changamoto ndogondogo zinazo wakabili ikwa ni pamoja na vyumba vya madarasa katika shule zao za Kata lakini bado wameendelea kutoa matokeo mazuri

Diwani wa Kata hiyo Bw. Emmanueli Ng’ata amekiri kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu japo jitihada zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha hakuna wanafunzi watakao somea nje

Hata hivyo Wilaya ya Chamwino kupitia kikao chake na wadau mbalimbali wa elimu wamekuja na kampeni ya nishike mkono Chamwino kwa lengo la kukusanya zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mabweni