Dodoma FM

Kamati ya Bunge ya haki maadili na madaraka ya Bunge yatoa ripoti Bungeni kuhusu shauri la mbunge wa Kawe

31 August 2021, 12:13 pm

Na;Yussuph Hans.

Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa Ripoti yake leo Bungeni Dodoma kuhusu shauri la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima Bunge na kutoa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge.

Akisoma taarifa yake mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema Shahidi alikiri kauli zote ni zake kwa asilimia mia moja na akisema ni mahubiri.

Kwa upande mwengine Kamati hiyo imetoa azimio kuhusu Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa kusema uongo kwamba mishahara ya Wabunge haikatwi Kodi hivyo Bunge limeazimia Silaa kutoahudhuria mikutano miwili mfululizo na kuondolewa kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika.

Aidha spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania Job Ndugai amesema lazima Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa aombe radhi hadharani kutokana na sakata lake la kusema kuwa wabunge hawakatwi kodi kwenye mishahara.

Mkutano wa nne wa Bunge la 12, Kikao cha Kwanza umeanza leo Agosti 31 jijini Dodoma kwa kipindi cha maswali na majibu pamoja na kupokea taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ya kuhojiwa kwa wabunge wa CCM, Jerry Silaa (Ukonga) na Askofu Josephat Gwajima (Kawe).