Dodoma FM

Wasichana walio katisha masomo yao kutokana na mimba za utotoni watakiwa kusaidiwa ili waweze kujisimamia kiuchumi

27 August 2021, 12:40 pm

Na;Yussuph Hans.

Jamii imetakiwa kuwasaidia Wasichana waliokatisha Masomo yao kutokana na Mimba za Utotoni ili waweze kujisimamia kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Asasi ya SAIKO Center Silvia Srriwa wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa Wasichana wanaopata mimba katika umri Mdogo wanakumbana na changamoto nyingi hivyo ni wajibu wa Jamii kuwasaidia.

Ameongeza kuwa jamii inapaswa kuongeza nguvu ili kupambana na mimba pamoja na ndoa za utotoni.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wanafunzi kufahamu namna gani wanafahamu madhara ya mimba za utotoni ambapo wamesema kuwa elimu inayotolewa shuleni inawasaidia kwa kiasi kikubwa kujilinda dhidi ya tabia hatarishi.

Tatizo la Ndoa na mimba za utotoni linatajwa kuwa chanzo moja wapo cha kusababisha umaskini katika familia na mataifa mengi katika Bara la Africa, Vile Vile tatizo hili la mimba za Utotoni limekuwa likichangia vifo vya mabinti wengi katika jamii zetu.