Dodoma FM

Kata ya Izava yasema ipo katika hatua za kutafuta ufumbuzi wa kisima kilicho haribika

27 August 2021, 1:37 pm

Na; Selemani Kodima.

Uongozi wa Kijiji cha Izava Kata ya Izava Wilayani Chamwino umesema upo katika mkakati wa kutafutia ufumbuzi suala la ukarabati wa kisima cha maji ili kuwaondolewa wananchi changamoto ya huduma hiyo.

Akizungumza na Taswira ya Habari Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Bw. Sokoine Mndewa amesema wameendelea kupambana ili kutatua changamoto ya maji ambayo imejitokeza mwaka huu baada ya kisima cha maji kuharibika.

Bw. Mndewa amesema hatua walizochukua mpaka sasa ni kukutana na wakala wa usambazaji maji na usafi na mazingira Vijijini RUWASA ambapo wameahidiwa kukutana na Waziri wa maji ili kuomba fedha za dharura kwa ajili ya ukarabati wa kisima hicho.

Amesema iwapo kisima hicho kitapokarabatiwa kitasaidia kusambaza maji katika kijiji cha Izava na kuchochea maendeleo ya wananachi wa Kijiji hicho.

Pamoja na hayo Kijiji cha Izava kina Kisima kimoja cha maji ambacho kimekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi walio wengi katika huduma ya maji safi na salama lakini changamoto kubwa kwa sasa ni uharibifu ambao umetokea mwaka huu na kusababisha huduma hiyo kusitishwa kwa wananchi