Dodoma FM

Foundation for disabilities hope (FDH)yaahidi kumsaidia Rhoda binti mwenye ulemavu

25 August 2021, 12:53 pm

Na; Mariam Matundu.

Foundation for disabilities hope imemtembelea binti Rhoda Batholomeo Nambali mwenye ulemavu wa akili pamoja na ulemavu wa viungo na kuahidi kumsaidia bima ya afya pamoja na kumtafutia wadau wengine watakao msaidia .

Afisa utawala wa taasisi hiyo Joyce Macha amesema wameona ni muhimu kufika nyumbani kwa wazazi wake na Rhoda ili kujionea mazingira ambapo kwa kuanza wamempelekea mahitaji madogo madogo kama mchele ,sukari ,mafuta ya kula pamoja na sabuni huku wakiahidi kushughulikia suala ya bima ya afya ya NHIF

Batholomeo Nambali ni baba mzazi wa binti huyo amekishukuru kituo cha redio cha Dodoma Fm pamoja na foundation for disabilities hope kwa kujitolea kumsaidia binti yake na kuwaomba waendelee kutenda wema huo.

Takribani mwezi mmoja sasa tangu kituo cha Dodoma fm redio kuripoti habari kuhusu changamoto anazozipitia binti Rhoda ambae ni mlemavu wa akili pamoja na viungo hali ambayo kwa mujibu wa daktari alisema ni muhimu kufikishwa hospitali kwa matibabu zaidi.