Dodoma FM

Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la polisi kutenda haki na kutimiza majukumu yake ipasavyo

25 August 2021, 1:08 pm

Na ; Fred Cheti.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani amelitaka jeshi la polisi nchini kutimiza majukumu yake imepasavyo kwa kutenda haki kwa jamii na kuepuka kutumia nguvu yake kuwakandakiza wananchi.

Mhe. Samia ametoa wito huo wakati akifungua kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka mmoja 2020-21 kwa Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi nchini, leo Agosti 25,2021 katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Aidha Rais Samia amewataka maafisa hao kuwaacha huru watu ambao wanahisi upelelezi wao hautokamilika katika kesi zao ili wakafaidi uhuru wao wakiwa nje na kama kesi haina mwelekeo watu hao waachiwe huru lakini kwa zile kesi ambazo wana hakika upelelezi utatimia ziharakiskishwe ili watu wasisote mahabusu.

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Inspekta Simon Sirro amesema kuwa hali ya ulinzi ya salama nchini imeendelea kuimarika kutokana na takwimu zilizopo licha ya kuwa bado uhalifu upo nchini
Igp. Sirro amesema jeshi la polisi lina mikakati mingi ya kupambana na uhalifu nchini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kukomesha vitendo hivyo.

Kikao hicho hufanyika kila mwaka ikiwa ni tahthimi ya utendaji kazi wa jeshi la polisi nchini ambapo leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani alikua mgeni Rasmi.