Dodoma FM

Wakazi wa Kawawa waiomba serikali kuwapelekea huduma ya umeme

19 August 2021, 1:31 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa kijiji cha Kawawa Kata ya Msanga Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwasaidia kufikisha huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili wananchi waweze kwenda na wakati.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema imekuwa ni muda mrefu wameshindwa kupatiwa huduma ya nishati ya umeme hivyo kuiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa kina.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw. Atanasio Mhimba amesema licha ya baadhi ya mitaa kuwa na umeme kwa kaya chache lakini bado changamoto ni kubwa kwa baadhi ya vitongoji.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw. Emmanueli Ng’ata amesema kuwa baadhi ya maeneo katika Kata yake yana umeme wa kujitosheleza lakini baadhi ya vitongoji vikiwa bado havija fikiwa na huduma hiyo

Wakala wa umeme Vijijini REA wameendelea na jitihada za kuhakikisha vijiji vyote Nchini vinafikiwa na huduma ya umeme kikamilifu