Dodoma FM

Nchi za Afrika zimeshauriwa kuwa na umoja ili kuepuka machafuko

17 August 2021, 11:19 am

Na; Benard Filbert.

Kufuatia machafuko makubwa katika nchi ya Afghanistan kati ya vikosi vya wanamgambo wa Taliban dhidi ya serikali, nchi za afrika zimeshauriwa kuwa na umoja ili kuepusha kujitokeza kwa hali kama hiyo.

Hayo yameelezwa na mhadhiri na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Bwana Paul Luislie wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mgogoro uliopo katika nchi ya Afghanistan.

Bwana Paul ameiambia taswira ya habari kuwa machafuko ambayo yametokea katika nchi ya Afghanistan ni dhairi bado hakuna utulivu wa kisiasa huku akidai hali hiyo imetokana na msaada wa kijeshi kutoka marekani kuisaidia serikali ya Afghanistan huku vikosi vya Taliban vikishindwa kufika muafaka na serikal ya nchi hiyo.

Bwana Paul amesema ingekuwa vyema wakati marekani imetuma vikosi vya kijeshi kutoa msaada inge egemea pande zote mbili kati ya serikali na vikundi vya Taliban ili kuleta suluhu kwani badala yake imesbabisha tatizo kuwa kubwa.

Mgogoro ambao umekuwa ukiikumba nchi ya Afghanistan dhidi ya wanamgambo wa Taliban umeibua sura mpya huku rais na makamu wa nchi hiyo wakiondoka ikulu huku zaidi ya watu laki tano wakiyakimbia makazi yao kwa kuhofia kupoteza uhai kutokana na mapigano.