Dodoma FM

Maafisa biashara watakiwa kuzingatia utoaji bora wa huduma

16 August 2021, 1:21 pm

Na;Mindi Joseph.

Maafisa Biashara wametakiwa kuzingata Utoaji wa huduma bora ili kuchangia wafanyabiashara kurasimisha biashara zao na kuingia katika zama za ushindani wa kibiashara.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya maafisa bisahara Afisa Mtendaji Mkuu BRELA Bw. Godfrey Nyaisa amesema baadhi ya wafanyabishara katika maeneo mbalimbali Nchini wanafanya Biashara pasipo kuwa na leseni hivyo sio jambo la busara kufungiwa biashara zao.

Ameongeza kuwa maafisa biashara wanajukumu la kuwaelimisha wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kuwa na leseni pamoja na kufanya ufatiliaji wa karibu kwa wafanyabiashara hao ili kuendelea kukuza uchumi wao na nchi.

Mafunzo hayo yanahusisha maafisa biashara kutoka mikoa mitatu Morogoro,siginda na Dodoma na yatafanyika kwa siku 5 jijini Dodoma.