Dodoma FM

Wakazi wa kijiji cha Kawawa walalamikia kukosa maeneo mbadala baada ya maeneo yao kutengwa kuwa hifadhi

11 August 2021, 12:13 pm

Na; Shani Nicolous.

Wananchi wa kijiji cha Kawawa kata ya msanga Wilaya ya Chamwino wamelalamikia kutokupewa maeneo mbadala ya kuishi baada ya kupimwa maeneo yao na kufanywa hifadhi ya wanyama.

Wakizungumza na Dodoma fm wananchi hao wamesema kuwa nikipindi kirefu sasa maeneo yao yamepimwa na hawakuridhishwa na malipo waliyokubaliana kwani waliambiwa watalipwa laki mbili na nusu kwa ekari moja.

Wamesema kuwa hali hiyo inawapa tabu hasa mtu akifariki wanalazimika kubeba maiti kwa njia ya mkokoteni wa ng”ombe au vitanda vya asili na kumzika eneo la mbali na kijiji hicho kwa kuogopa mikataba ambayo tayari ilifanyika.
Wameiomba serikali ku kuingilia suala hilom kwani wanahofia familia kwa maana ya watoto baadaye wataishi maisha magumu na kukosa elimu kupitia changamoto hizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho amesema kuwa anafahamu changamoto hiyo ya wananchi kutokuridhishwa na malipo na kwakuwa zoezi hilo lilifanywa na serikali kuu wameshindwa kuliingilia

Bwana Emmanuel Yohana Ng”ata ni Diwani wa kata hiyo ameiambia Dodoma fm kuwa wakati maeneo hayo yanapimwa yeye hakuwa madarakani lakini anafahamu changamoto hiyo na anaahidi kuwa pambania ili kupata haki zao.

Baadhi ya maeneo jijini Dodoma bado yanakumbana na changamoto za migogoro ya ardhi pamoja naserikali kufanya taratibu mbalimbali za kutatua changamoto hizo kupitia kampeni ya zero migogoro ya ardhi.