Dodoma FM

Ongezeko la watu katika kijiji cha Sunya Kiteto lapelekea shida ya maji kukikabili kijiji hicho

11 August 2021, 12:35 pm

Na; Selemani Kodima.

Imeelezwa kuwa Ongezeko la watu na mahitaji ya maji katika kata ya Sunya wilayani kiteto imesababisha kuongezeka kwa changamoto ya maji katika baadhi Vijiji hususani Kijiji cha Sunya.

Hayo yameelezwa na Baadhi ya Wanakijiji wa kijiji cha Sunya wakati wakizungumza na Taswira ya Habari kuhusu gharama wanazotumia kununua maji pamoja na adha wanazopitia kutokana na changamoto hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Sunya Bw Chembe Emmanuel….amesema kuwa changamoto ya maji ni kubwa katika eneo hilo licha ya uwepo wa kisima kimoja cha maji chenye vituo viwili lakini bado hali ni mbaya kwa wakaazi wa eneo lake.

Naye Diwani wa kata ya Sunya Bw Muss Brayton amesema kwa mujibu wa bajeti ya mwaka fedha 2021/22 kata yake imetengewa fedha kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji katika maeneo ambayo hayana chanzo chochote cha maji.

Pamoja na hayo amewataka wakazi wa Sunya kuwa na subira kutokana na ahadi waliyopewa na RUWASA kwa ajili kutumia chanzo cha maji katika kijiji cha Chang’ombe ili kufanikisha kupunguza changamoto ya hiyo.