Dodoma FM

Wakazi wa Mkanana walalamikia kukosa maji safi na salama

10 August 2021, 11:56 am

Na; Selemani Kodima.

Licha ya uwepo wa chemchem za maji katika kijiji cha Mkanana bado Changamoto ya Maji imeendelea kuwa kilio kwa wakazi wa eneo hilo hali ambayo msimu wa kiangazi inakuwa mara dufu.

Baadhi ya wananchi wakizungumza na Taswira ya Habari wamesema kuwa tatizo la maji huanza kuwa kubwa kuanzia Msimu wa kiangazi kutokana na baadhi ya chemchem kupungua maji hivyo kuwalazimu kutumia maji yasio safi na salama.

Hekima na Medicko Julias ni Wakazi wa kijiji cha Mkanana wamesema hali ya maji kwa sasa ni Tabu kwao kutokana na athari wanazozipata kupitia maji hayo ikiwemo kukosa Usalama wa kutosha.

Kutokana na Changamoto hiyo,Diwani wa Kata ya Chitemo Bw DONALD EDWARD JEREMIA amekiri kuwepo kwa changamoto ya maji katika kijiji cha Mkanana hususani msimu wa kiangazi .

Amesema Jitihada ambayo wamechukua ni kufikisha changamoto hiyo kwenye Idara ya Maji huku akiwataka wananchi kuendelea kuyatumia maji yaliyopo katika chemchem ya kijiji kwa kuzingatia usalama wa maji.

Pamoja na hayo amewataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati huu ambao wanasubiri kutatua changamoto ya maji katika kata chitemo.