Dodoma FM

Mifumo duni ya kilimo cha mtama yapelekea uzalishaji kuwa hafifu wilayani Kongwa

10 August 2021, 12:37 pm

Na; Shani Nicolaus .

Mtama – 5kg – Dalima Foods

Imeelezwa kuwa kutokuzingatia upandaji wa mbegu bora za mtama kwa baadhi ya wakulima katika wilaya ya Kongwa inachangia uzalishaji duni wa zao hilo hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wakulima.

Hayo yamesemwa na afisa kilimo pamoja na mratibu wa zao la mtama katika wilaya Kongwa Bi Amina Msangi wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema wakulima wengi katika wilaya hiyo wamekuwa wakitumia mtama ambao ni chakula kwa ajili ya kupanda kitu ambacho sio sawa.

Amesema kitaalamu haitakiwi kupanda mbegu ambazo zimetoka shambani kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita na badala yake inatakiwa watumie mbegu mpya.

Kadhalika amesema ili kuleta kilimo chenye tija kwa wakulima katika wilaya ya Kongwa wamekuwa wakiwaunganisha na taasisi mbalimbali za kifedha ili kupata mikopo ya kuendeleza kilimo chao.

Maziwa Ally Maziwa ni afisa usimamizi wa manunuzi ya mtama katika eneo la kibaigwa wilaya ya Kongwa amesema wamekuwa na mchango mkubwa ikiwepo kutoa elimu kwa wakulima kutumia mbegu bora ili kuleta ushindani wa zao la mtama.

Serikali inahimiza wakulima kutumia pembejeo za kisasa ikiwepo mbegu bora ambazo zinashauriwa na maafisa kilimo ili kulima kilimo chenye tija.