Dodoma FM

Jamii imetakiwa kuto puuza swala la kuandika wosia ili kuepusha changamoto zinazo jitokeza katika ugawaji mali

29 July 2021, 10:30 am

Na; Shani Nicolous.

legalavenue⚖ Instagram posts - Gramho.com

Jamii imetakiwa kutokupuuza suala la kuandika wosia kuhusiana na masuala ya mirathi kwani kumekuwa na changamoto nyingi zinazojitokeza katika ugawaji wa mali za marehemu.

Akizungumza na Dodoma fm kupitia kipindi cha Dodoma live msaidizi wa kisheria kutoka shirika la Just kata ya Kondoa Salimu Salimu amesema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakifikiria kuandika wosia ni kama kutabiri kifo lakini ni msaada moja wapo katika kurahisisha taratibu za mirathi baada ya kifo cha muhusika.

Amesema kuwa Wosia huandikwa na watu wazima ambao tayari wapo kwenye familia hivyo ni vema wakazingatia hilo na kuchukulia umuhimu wa kuandika wosia kwa taratibu sahihi.

Aidha ameongeza kuwa kuna faida nyingi za kuandika wosia kwani mali zitagawanywa kulingana na maelekezo amabayo yaliachwa na marehemu na hivyo kuepusha ugomvi na mitafaruku mbalimbali amabyo ingetokea kutoka katika familia na ukoo mzima.

Kwa upande wake Habiba Suluta ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kutoka Wilaya ya Kondoa amesema kuwa ni vema watu wakazingatia kuacha wosia katika familia zao lakini pia pindi tatizo la mirathi likitokea wasisite kufika katika ofisi za kisheria kwaajili ya kutatua changamoto zao.

Baadhi ya familia zimekuwa zikigombana na kutengeneza chuki pindi tu linapotokea suala la kugawana mali za marehemu wakati mwingine kufikia hatua yakutengeneza vita hata kuuana , jamii bado inahitaji elimu yakutosha juu ya wosia ili kuondoa migogoro isiyo yalazima katika jamii.