Dodoma FM

Ukosefu wa shule ya sekondari katika kata ya KK wapelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu

26 July 2021, 10:48 am

Na; Benard Filbert.

Ukosefu wa shule ya sekondari katika kata ya KK imetajwa kuwa changamoto kwa wanafunzi wa kata hiyo hali inayowalazimu kutembea umbali wa kilomita 7 hadi kata ya BUSI kwa ajili ya masomo.

Hayo yameelezwa na wakazi wa kata hiyo wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya upatikanaji wa elimu hususani ngazi ya sekondari.

Juma ally ni miongoni mwa wakazi hao ameiambia taswira ya habari kuwa wanafunzi wote wa sekondari katika kata hiyo wanalazimika kuondoka saa kumi alfajir kwenda kata jirani ambapo kuna shule ya sekondari jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Taswira ya habari imezungumza na diwani wa kata ya KK bwana Mchana Issa amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo imekuwa kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa kata ya KK hali inayopelekea wananfunzi wa kata hiyo kwenda kusoma kata jirani.

Amesema mkakati uliopo hivi sasa wameanza ujenzi wa shule ya sekondari KK kwa nguvu za wananchi lakini kumetokea mgogoro baadhi ya wananchi hawataki shule hiyo ijengwe katika eneo la makao makuu ya kata ya KK.

Vijiji vingi nchini vimekuwa vikikumbwa na changamoto baadhi ya wanafunzi kutembea umbali mrefu hali ambayo inasababisha kuchukua muda wa ziada kufika katika shule husika huku serikali ikiwa na juhudi madhubuti kutatua changamoto hiyo.