Dodoma FM

Wakazi wa Matongoro wakabiliwa na uhaba wa wahudumu wa afya

23 July 2021, 12:41 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Matongoro Wilaya ya Kongwa wanakabiliwa na uhaba wa watumishi katika huduma ya afya pamoja na nyumba za watumishi hao.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesena wanakabiliwa na uhaba wa manesi licha ya kuwa na daktari mmoja mmoja katika vituo vingi pamoja na ukosefu wa nyumba za watumishi hao

Mwenyekiti wa kijiji cha Mranje Bw. Elisha Mpanda amekiri kuwepo kwa adha nyumba ya mganga mkuu huku wakiwa na daktari mmoja na nesi mmoja nakuiomba serikali kuwasaidia kuwaongezea watumishi wa afya.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Jeremiah Mkanda ameeleza jitihada walizoendelea kuzichukua kwa Kata nzima ili kuhakikisha wana boresha huduma hiyo kwa wananchi.

Serikali na wananchi wa Kata ya Matongoro inayoundwa na jumla ya vijiji vitatu amabavyo ni Norini ,Mranje pamoja na kijiji cha Matongoro wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanapunguza changamoto za kata hiyo