Dodoma FM

Wakazi wa Masinyeti waishukuru Dodoma fm kwa kuwasaidia kutatuliwa kero ya maji

20 July 2021, 12:20 pm

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa kijiji cha Masinyeti kata ya Iduo wilayani Kongwa wameishukuru Dodoma redio kwa juhudi kubwa waliofanya ya kuripoti changamoto ya adha ya maji katika eneo hilo na hatimaye kuchimbiwa kisima cha maji na Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini RUWASA.

Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wamesema juhudi ambazo zimefanywa na Dodoma redio ni Msaada tosha kwao hivyo waendelee kushirikiana na wananchi katika kuwasaidia kuripoti changamoto zao.

Edna Miambe na John Reheni ni wakazi wa kijiji cha Masinyeti wamesema hatua za kufanikisha upatikanaji wa maji katika kijiji hicho itasaidia kuondoa baadhi ya changamoto za maji ambazo zilisababisha umbali wa upatikanaji wa huduma hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Masinyeti Bw Saimoni Mwimbano amesema hatua ya kwanza ya uchimbaji imefanyika na sasa wanasubiri hatua ya pili ambayo itahusishwa ujenzi wa tanki na usambazaji wa maji.

Amesema ni Faraja kwa kijiji cha Masinyeti kuona RUWASA ikitekeleza mpango wa uchimbaji wa kisima cha maji ndani ya eneo hilo hivyo uwepo wa maji utasaidia katika hatua ya Ujenzi wa za hanati pamoja nashughuli za kimaendeleo .

Mafanikio haya yamekuja baada ya kituo hiki kuendelea kuwa sehemu ya kufuatilia na kuandaa vipindi vinavyoangazia changamoto kadhaa zinazowakabili wananchi hususani maeneo ya Vijijini.