Dodoma FM

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameisimamisha kazi kampuni ya upimaji wa ardhi eneo la Michese

19 July 2021, 9:53 am

Na ;Benard Filbert.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Antony Mtaka ameisimamisha kampuni ya upimaji wa ardhi ambayo imekuwa ikitekeleza kazi zake  eneo la kata ya Mkonze.

Mtaka ametoa agizo hilo baada ya kusikiliza kero za wananchi wa mitaa mbalimbali ya Michese  ambao  wamesema kampuni hiyo ilikuwa chanzo cha migogoro ya ardhi hivyo hivyo wameiteua kamati maalumu ya mkoa ,jiji pamoja na Wizara  kufanyakazi ambazo zilikuwa zinafanywa na kampuni hiyo.

Akitoa malekezo ya Serikali Mtaka ameitaka halmashauri ya jiji kufanya uhakiki wa makampuni ya upimaji wa ardhi kama ina migogoro  ili kuepusha kufanya malipo huku wakiwa na migogoro ya ardhi.

Kwa upande  mwingine Mtaka amesema kwa kuzingatia umuhimu wa zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi kupitia kampeni ya zero migogoro ya ardhi wameongeza siku 10 kwa ajili ya kuendelea kuwahudumia wananchi katika maeneo ambayo walipata migogoro mingi.

Hata hvyo amewataka wananchi wasiuze maeneo yao wakati huu ambao serikali kupitia kamati maalumu wanaendelea kushughulikia changamoto zao .

Mtaka amesema kupitia Zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ambalo lilianza tarehe 5 mwezi huu mpaka Leo,Kamati  imefanikiwa kukutana na migogoro ya ardhi 2382 huku zaidi ya migogoro 500 imeamuliwa.