Dodoma FM

Wakazi wa Songambele A waishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kwaajili ya ujenzi wa zahanati

16 July 2021, 11:08 am

Na; Victor Chigwada.

Wananchi katika Kata ya Songambele A wameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya .

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kuwepo kwa Zahanati kutarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu hasa kwa akina mama wajawazito .

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. William Makoli amesema tayari wameanza kusafisha eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho baada ya kupewa fedha na Serikali milioni mia nne huku akiomba kuongezewa wahudumu wa afya.

Diwani wa Kata ya Songambele Bw. Patrick Meso amesema kuwa kuna Vijiji vitatu ambavyo havina zahanati huku tayari wameanza ujenzi kwa hamasa ya wananchi pamoja na kuishukuru Serikali kwa ujenzi wa kituo cha afya ambao utapelekea kupunguza adha kwa wananchi hao.

Serikali imekuwa ikiweka kipaumbele katika kuboresha huduma za afya Nchini ikiwemo ujenzi wa zahanati, vituo vya afya hosptali, wahudumu wa afya pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba zikiwemo madawa na vifaa tiba katika vituo hivyo