Dodoma FM

Wanaume wilayani Kongwa watakiwa kutambua majukumu yao katika familia

14 July 2021, 1:49 pm

Na; Benard Filbert.

Wanaume katika kata ya Chiwe wilayani Kongwa wametakiwa kuepuka kutelekezea wanawake majukumu ya familia ikiwemo kusomesha watoto na badala yake washiriki kwa pamoja.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Chiwe Bw. Dastan Chinyali wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amebainisha kuwa kuna baadhi ya wanaume katika kata hiyo wamekuwa wakiwaachia wanawake majukumu makubwa katika familia kitu ambacho si sahihi.

Amesema mara kadhaa wamekuwa wakipokea kesi za wanawake wakilalamika juu ya wanaume kutelekeza majukumu ya familia ikiwemo kusomesha watoto.

Ameongeza kuwa wamekuwa wakiendelea kuelimisha jamii katika mikutano ya hadhara kwani kila mwanaume anao wajibu wakutimiza majukumu ya msingi katika familia.

Baadhi ya wananchi wakizungumza na taswira ya habari wamesema mwanaume anawajibu wakutimiza mahitaji ya msingi katika familia.

Ni wajibu wa wanandoa wote kushiriki kwa pamoja katika matunzo ya familia ikiwemo kusomesha watoto pamoja na shugjhuli zingine kwa ustawi wa famila.